Mwanzo›Dhikri›Dua ya wakati wa kusujudu (19)
Dua ya wakati wa kusujudu
دعاء السجود · Hisnul Muslim · 7 dhikri
- dhikri 1((سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى)) ثلاث مرَّاتٍ.Ametakasika Mola wangu aliye juu. (Atasema hivo mara tatu)
- dhikri 2((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي)).Kutakasika ni kwako, Ewe Mwenyezi Mungu Mola wetu, na sifa njema zote ni zako, Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe.
- dhikri 3((سُبوحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ الْمَلَائِكَةِ وَالرُّوحِ)).Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriil.
- dhikri 4((اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، سَجَدَ وَجْهِيَ لِلَّذِي خَلَقَهُ، وَصَوَّرَهُ، وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ، تَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسنُ الْخَالِقينَ)).Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia aliyeuumba na akautia sura na akaupasua usikizi wake na uoni wake,…
- dhikri 5((سُبْحَانَ ذِي الْجَبَرُوتِ، وَالْمَلَكُوتِ، وَالْكِبْرِيَاءِ، وَالْعَظَمَةِ)).Ametakasika Mwenye Utawala na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu.
- dhikri 6((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ: دِقَّهُ وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، وَعَلاَنِيَّتَهُ وَسِرَّهُ)).Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na mwisho, za wazi na za siri.
- dhikri 7((اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ، لاَ أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ، أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ)).Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako unihifadhi na wewe, mimi…
Sikiliza · Sauti ya Hamad al-Duraiham