MwanzoDhikriTakbira anaporusha kila jiwe katika jamarah (nguzo)dhikri 1

Takbira anaporusha kila jiwe katika jamarah (nguzo) — dhikri 1

التكبير عند رمي الجمار مع كل حصاة · Hisnul Muslim · 1 / 1

Soma · SikilizaFaili la PDF

((يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ عِنْدَ الْجِمَارِ الثَّلاَثِ، ثُمَّ يَتَقَدَّمُ، ويَقِفُ يَدْعُو مُسْتَقْبِلَ الْقِبلَةِ، رَافِعاً يَدَيْهِ بَعْدَ الْجَمْرَةِ الْأُولَى وَالثَّانِيَةِ. أَمَّا جَمْرَةُ الْعَقَبَةِ فَيَرْمِيهَا وَيُكَبِّرُ عِنْدَ كُلِّ حَصَاةٍ وَيَنْصَرِفُ وَلاَ يَقِفُ عِنْدَهَا)).

Alikuwa Mtume (s.a.w) kila anaporusha kijiwe katika Jamarah (nguzo) tatu anasema: ''Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.'' ....Anapomaliza kurusha vijiwe saba katika Jamarah (nguzo) ya kwanza, alikuwa anasogea mbele kidogo, anasimama kuelekea Qiblah, hali ya kuwa ameinua mikono yake, kisha anaanza kumuomba Mwenyezi Mungu. Alikuwa akifanya hivo katika Jamarah ya kwanza na ya pili tu, ama (Jamara) ya tatu alikuwa hasimami bali akimaliza anaondoka.

Sikiliza · Sauti ya Hamad al-Duraiham

Dhikri · 15 lugha